Sunday, March 17, 2013

HEALTH TIPS: DIABETES MELLITUS-KISUKARI



DIABETES MELLITUS –KISUKARI.

Diabetes mellitus has now become a most feared disease in urban areas, and this has largely attributed by dramatic changes in life styles of people.
It’s most feared as it has no definitive treatment, use you acquire the condition, the hope remains in palliatives, which do nothing than controlling blood sugar, so as to halt the speed of progression of disease into devastating complications.
Having diagnosed with diabetes mellitus, and especially when it reaches the criteria of using medications, it mean nothing but to spend entire life in medications! This has psychological and economic implications.
There are two types of DM,typeI and  DM typeII. Here I will focus on DMII as it occurs in adults and there are some measures to take, for the sake of being on safe side.

KISUKARI NI NINI?

Mtu  anapokua na kisukari maana yake ni kwamba sukari kwenye damu ni nyingi kuliko kiwango cha  kawaida.
Kwa hali ya kawaida sukari yapaswa kua katika  vipimo vya 3.5mmol/L mpaka 11.10mmol/L endapo ikiwa zaidi  11.1mmol/L,hili ni tatizo.

Dalili  nyingine za kisukari ni pamoja na 

·         Kiu ya maji ya mara kwa mara-polydispia (kawaida  mtu hunywa maji lita 2 kwa siku)
·         Hamu kubwa ya chakula/kula sana-polyphagia
·         Kukojoa mara kwa mara-polyuria (kwa usiku kuamka zaidi ya mara tatu ajiri ya kukojoa)
·         Kupungua uzito-weight loss
·         Kupoteza nguvu ya macho-blurred vision
·         Kupata maambukizi ya fangasi mdomoni,vidoleni na sehemu za siri.-candindiasis

Ukiona dalili hizi ni heri kuwahi mapema kituo cha afya au hospitali na kucheki sukari.au kama una glucometer nyumbani check


MADHARA YA KISUKARI NI NINI?

impotence-ndoa hatarini
·        Kupata shinikizo la damu/high blood pressure
·         Waweza kupata kiharusi (stroke)  
·         Kupoteza nguvu ya macho/upofu
·         Figo kupata madhara,isipo tibiwa figo hufa kabisa
·         Kupoteza nguvu za kiume/hamu ya tendo la ndoa
·         Kupata ganzi miguuni na mikoni
·         Vidonda visivyo pona/vidonda ndugu ambavyo hupelekea miguu/mguu kutatwa (amputation)






KISUKARI HUPATIKANA  VIPI

Munganiko wa vitu viwili kwa pamoja (synergism) hupelekea mtu kupata kisukari.

1.      Urithi wa chembechembe toka wa kizazi (genetic predisposition from 1st degree relatives)
·         Kama kuna ndugu yako wa karibu kwa damu au mzazi mwenye tatizo la sukari,uwezekano unakua mkubwa nawe kupata-1st degree relative


2.      Mazingira ya maisha (life style).
·         Uzito usioendana na kimo/urefu-BMI.Normal range 18-25 calculated by =weight in kg/height  in meter  squre. Tumia hata simu yako kama ni adroid.
au waist circumfarence zaidi ya 88cm kwa wanawake na 102cm kwa wanaume

·         Kula vyakula vyenye mafuta ya cholesterol/vinywaji vyenye sukari
·         Maisha ya kukaa kaa pasipo mazoezi  (sedentary life style)
·         Pombe/ulevi
·         Matibabu yaambatanayo na vidonge Fulani (thiazides,beta blockers,anti psychotic,statins etc)
·         Mimba


Muunganiko wa sababu za mwanzo na hizi za pili hupelekea kongosho kushindwa kuzalishaa vichocheo insulin au mwili kushindwa kurespond kwa vichocheo hivyo hata kama vina zalishwa. Hivyo mtu kupata kisukari.
Hapa hatuwezi kujikinga na sababu zilizopo katika kundi la 1,ila tunaweza kuziepuka hizo katika kundi la2.


NANI ANATAKIWA KWENDA KU SCREEN AJIRI YA KISUKARI?


 
kipimo cha sukari

ü  Mwenye umri wa miaka 45
ü  Mjamzito
ü  Mwenye pressure zaidi ya 140/90
ü  Mwenye BMI zaidi ya 30
ü  Mwenye ndugu wa karibu,ambae ana kisukari
ü  Mwenye maradhi ya ovaries

TUNAJIKINGA VIPI NA KISUKARI?
·         Mazoezi ya mapangilio-regular exercise
·         Chakula chenye mpangilio-health diet
·         Kupunguza uzito kulingana na vimo vyetu
·         Kupunguza pombe/au kuacha kabisa.


***************************************************
Weka maoni yako.

1 comment: