Sunday, September 16, 2012

KISA CHA WANAFUNZI 5 WA CHUO

Wanafunzi watano wa chuo kikuu kimoja
hapa nchini walikuwa wanatakiwa
wafanye mtihani siku ifuatayo. Wale
wanafunzi wakanywa pombe mpaka saa
nane usiku. Siku ya mtihani wote wakawa na uchovu
wa hangover,hivyo wakashindwa kwenda
kufanya mtihani. Wakatunga uongo wa kuenda
kumwambia Lecturer wa somo
husika.Wakaenda kumdanganya Lecturer
kuwa walishindwa kufanya mtihani kwa
sababu jana walienda harusini na wakati
wanarudi gari lao likapata pancha na wakavamiwa na majambazi wakawapiga
na kuwaibia. Yule Lecturer akakubali na akawapa siku
tatu za kujiandaa kwa Special exam. Siku ya mtihani special,Lecturer aliwapa
ma paper na kuwasimamia mwenyewe.
Mwongozo wa mtihani ulikuwa kama
ufuatavyo; 1.Mtihani huu ni kwa wanafunzi watano. 2.Majibu yao yote yafaa yawe
sawa...yakiwa tofauti watapata zero na
kufeli. 3.Mtihani huu una maswali matano na
yote lazima yajibiwe. Maswali ya mtihani yalikuwa hivi: 1.Harusi ilifanyika sehemu gani? 2.Gari mliotumia mpaka mkapata pancha
inaitwaje? 3.Ajali ilitokea eneo gani? 4.Nani alikuwa dereva? 5.Tairi ipi ilipata pancha...ya mbele au
nyuma? NAWATAKIA MTIHANI MWEMA.

No comments:

Post a Comment